You are here

Namna ya kuswali

×

Error message

Deprecated function: Function create_function() is deprecated in views_php_handler_field->pre_render() (line 202 of /var/www/drupal7-websites/sites/all/modules/contrib/views_php/plugins/views/views_php_handler_field.inc).

 1. Nia:

Nia ni sharti la swala kuwa sahihi, kwa maana ya mtu kukusudia kwa moyo wake kumuabudu Allah kwa kuswali, huku akijua kwamba swala anayoswali ni Magharibi kwa mfano au Isha. Haitakiwi na sheria kuitamka hii nia, bali makusudio ya moyoni na akilini ndio yanayotakiwa. Kuitamka Nia ni jambo ambalo hilo halikuthibiti kunukuliwa kwa Mtume,swallalahu alayhi wasalam, wala maswahaba wake watukufu.

 1. Atasimama wima kwa ajili ya swala na kusema: 

(Allahu Akbar). Atanyanyua mikono yake mpaka usawa wa mabega yake au juu yake huku matumbo ya viganja vya mikono akiyaelekeza upande wa Kibla.
Takbira haiwi sahihi isipokuwa tu kwa tamko hili la (Allahu Akbar). Maana yake ni kumtukuza na kumuadhimisha Allah. Allah ni mkubwa zaidi kuliko kila kisichokuwa yeye. Ni mkubwa zaidi kuliko dunia pamoja na starehe zote na matamanio yote yaliyomo humo. Tunaziweka kando starehe zote hizo na tunaelekea kwa Allah mkubwa, mtukufu katika swala kwa nyoyo zetu na akili zetu huku tukiwa wanyenyekevu.

 1. Baada ya Takbira, atauweka mkono wake wa kulia juu ya wa kushoto, juu ya kifua chake. Atafanya hivyo mara zote katika kusimama kwake.
 1. Atasoma dua ya kuanzia swala, ikiwa ni jambo linalopendekezwa: (Sub-haanakallaahumma Wabihamdik, Watabaarakasmuk, Wataalaa jadduk, Walaa ilaaha ghairuk).
 1. Atasoma: (Auudhu billaahi Minash-shaitwaanir-rajiim). Hii ni dua ya kuomba kinga. Maana yake ni kwamba: Ninamkimbilia Allah na kumuomba anikinge na uovu wa shetani.
 1. Atasoma: (Bismillahir-rahmaanir-rahii). Maana yake ni: Ninaanza (kuswali) nikiomba msaada na nikiomba baraka kwa jina la Allah.
 1. Atasoma suratul faatiha ambayo ni sura tukufu sana katika kitabu cha Allah.
 • Allah amempa Neema Mtume wake kwa kuiteremsha sura hii na kusema kwamba: «Na, kwa yakini kabisa, tumekupa wewe aya saba katika aya zinazokaririwa, na Qur’ani Tukufu». (Sura Alhijri, aya 87). Imeitwa hivyo kwakuwa ni aya saba ambazo watu wanazirudiarudia mara nyingi kila siku. 
 • Ni wajibu kwa Muislamu kujifundisha sura hii, kwa sababu kuisoma ni nguzo katika swala, kwa mtu anayeswali peke yake au maamuma katika swala ambayo imamu katika hiyo hasomi kwa sauti ya juu.
 1. Sheria inamtaka mwenye kuswali baada ya kusoma suratul faatiha au kuisikiliza katika kisomo cha imamu aseme (Aamiin). Maana yake ni: Ewe Mola jibu maombi..
 1. Baada ya Alfaatiha katika rakaa mbili za mwanzo atasoma sura nyingine au aya za sura nyingine. Ama katika rakaa ya tatu na ya nne, atatosheka na kusoma sura Alfaatiha tu.
 • Kusoma sura Alfaatiha na Qur’ani nyingine baada yake kunakuwa kwa sauti ya juu katika swala ya Alfajiri, Magharibi na Isha. Kusoma kunakuwa kimya kimya katika swala ya Adhuhuri na Alasiri. 
 • Ama nyiradi nyingine za swala zinasomwa kimya kimya.

 1. Halafu atasoma Takbira kwa ajili ya kurukuu huku akinyanyua mikono yake mpaka mkabala na mabega yake au juu zaidi, akiyaelekeza matumbo ya viganja vya mikono yake upande wa Qibla, kama alivyofanya katika Takbira ya kwanza.
 1. Atarukuu; kwa kuuinamisha mgongo wake akielekea upande wa Qibla, na mgongo na kichwa chake vitakuwa vimenyooka. Ataweka mikono yake juu ya magoti yake na kusema: 

(Subhaana Rabbiyal-adhiim). Inapendekezwa kurudia tasbihi hii mara tatu. Rukuu ni mahali pa kumtukuza na kumuadhimisha Allah Mtukufu.

Maana ya (Sub-haana Rabbiyal-adhiim) ni: Ninamtakasa Allah kwamba hana upungufu. Nayasema haya na ilhali nimerukuu, nimeinama, nikiwa mnyenyekevu kwa Allah Mtukufu.

 1. Atanyanyuka kutoka katika kurukuu na kwenda kusimama huku akinyanyua mikono yake mpaka mkabala wa mabega yage huku matumbo ya viganja vya mikono yake yakielekea upande wa Qibla, kama ilivyotangulia kuelezwa, na atasema: 

(Samiallahu Liman-hamidah) akiwa imamu au akiwa maamuma. Halafu wote watasema: (Rabbanaa walakal-hamdu). Inapendekezwa kwake kuongeza na kusema baada yake: (Hamdan kathiiran, Twayyiban, Mubaarakn-fiihi. Mil-assamaawaati Wamil-al-ardhi. Wamil-amaa Shi-ita Min-shain Baadu).

 1. Baada ya hapo atainama kwenda chini huku akileta Takbira na kusujudu kwa kutumia viungo saba.

 Viungo hivyo ni: paji la uso pamoja pua, viganja (vyote miwili), magoti (yote mawili) na miguu (yote miwili). Inapendekezwa kwake tumbo asiligusishe na mapaja, mapaja asiyagusishe na miguu katika kusujudu kwake. Pia mikono yake ainyanyue isiguse ardhi.

 1. Katika kusujudu kwake atasema: (Sub-haana Rabbiyal-aalaa). Inapendekezwa kurudia mara tatu.

Maana ya (Sub-haana Rabbiyal-aalaa) ni: Ninamtakasa Allah aliye juu kabisa katika utukufu wake na hadhi yake, na aliye juu kabisa juu ya mbingu zake kwamba ameepukana na upungufu na kasoro zote. Katika hilo kuna kumzindua mwenye kusujudu aliyegusa ardhi juu ya udhaifu na unyonge ili akumbuke tofauti iliopo kati yake na kati ya Muumba wake aliye juu sana, na kwa ajili hiyo, awe mtiifu na mnyenyekevu kwa Mola wake.

Kusujudu ni katika sehemu adhimu sana za kumuomba Allah. Baada ya nyiradi za wajibu, Muislamu ataomba kheri za dunia na akhera azitakazo. Mtume,swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Sehemu ambayo mja anakuwa karibu sana na Mola wake ni pale anapokuwa amesujudu. Kwa hiyo, ombeni sana». (Muslim, Hadithi Na. 482).

 1. Halafu atasema: (Allahu Akbar)

na kukaa kati ya sijda mbili. Inapendekezwa kwake kuukalia mguu wake wa kushoto na kuusimamisha mguu wake wa kulia. Ataweka mikono yake juu ya sehemu ya mbele ya mapaja yake katika sehemu inayofuatia magoti

 • Inapendekezwa katika vikao vyote vya swala aina hii ya ukaaji, isipokuwa tu katika Tashahudi ya mwisho. Katika Tashahudi hiyo ya mwisho, inapendekezwa kwake pia kunyanyua mguu wa kulia, lakini atauchomoza mguu wa kushoto utokeze chini ya mguu huo wa kulia, na makalio yake yakikalia ardhi.
 1. mbili: (Rabbigh-firlii). Inapendekezwa kurudia mara tatu.
 1. Halafu atasujudu mara ya pili kama kusujudu kwake kwa mwanzo.
 1. Halafu atanyanyuka akitoka kwenye kusujudu kwa mara ya pili akienda kwenye kusimama huku akisema: (Allahu Akbar).
 1. Na ataswali rakaa ya pili sawa sawa kama ya kwanza.
 1. Baada ya kusujudu kwake mara ya pili katika rakaa ya pili, atakaa kwa ajili ya Tashahudi ya Kwanza, na kusema: 

(Attahiyyaatu Lillah, Wasswalawaatu, Wattwayyibaatu. Assalaamu Alaika Ayyuhannabiyyu Warahmatullahi Wabarakaatuh. Assalaamu Alainaa Wa-alaa Ibaadillahiswaalihiina. Ash-hadu Allaa-ilaaha Illallahu Wa-ash-hadu Anna Muhammadn Abduhuu Waras

 1. Halafu atasimama kwa ajili ya sehemu iliyobaki ya swala yake ikiwa swala hiyo ni ya rakaa tatu au nne, 

isipokuwa tu katika kusoma kwake atatosheka na kusoma suratul faatiha tu katika rakaa ya tatu na ya nne.

 • Ama swala ikiwa ya rakaa mbili kama ya Alfajiri, ataleta Tashahudi ya Mwisho, kama itakavyokuja kuelezwa.

 1. mara ya pili atakaa kwa ajili ya Tashahudi ya Mwisho pamona kuongeza kumsalia Mtume kwa namna ifuatayo: 

(Allaahumma Swalli Alaa Muhammad. Wa Alaa Aaali Muhammad. Kamaa Swallaita Alaa Ibraahiim Wa Alaa Aali Ibraahiim. Innaka Hamiidun Majiid. Wabaarik Alaa Muhammad Wa Alaa Aali Muhammad. Kamaa Baarakta Alaa Ibraahiim Wa Alaa Aali Ibraahiim. Innaka Hamiidun Majiid).

 • Baada ya hayo ni sunna kwake kusema: (Auudhu Billahi Min-adhaabi Jahannam. Wamin-adhaabil-qabri. Wamin-fitnatil-mahyaa Walmamaat. Wamin-fitnatil-masiihid-dajjaal). Na ataomba jambo apendalo.
 1. Halafu atageuka upande wa kulia akisema: (Assalaamu Alaikum Warahmatullaah). Halafu atageuka upande wa kushoto na kusema hivyo hivyo.

Kwa kutoa salamu Muislamu anakuwa amekamilisha swala yake, kama Mtume,swallalahu alayhi wasalam, alivyosema kuwa: «Mwanzo wake ni kuleta Takbira na mwisho wake ni kutoa salamu). (Abudaud, Hadithi Na. 61. Tirmidhiy, Hadithi Na. 3). Maana ni kwamba mtu anaingia katika swala kwa kuleta Takbira ya Kwanza na anamaliza kwa kutoa salamu.. 

 1. Inapendekezwa kwa Muislamu baada ya kutoa salamu ya swala ya faradhi asemee: 
 1. (Astaghfirullah mara tatu – Namuomba msamaha Allah).
 2. Na atasema: (Allaahumma Antassalaam. Waminkassalaam. Tabaarakta Yaadhaljalaal Wal-ikraam). (Allahumma Laamaania Limaa Aatwaita. Walaa Muutwiya Limaa Manaa’ta. Walaa Yanfau Dhaljaddi Minkaljaddu).
 3. Halafu atasema: (Sub-haanallah). Atarudia rudia mara 33, na (Alhamdu Lillah) mara 33, na (Allaahu Akbar) mara 33. Atakamilisha mara mia moja kwa kusema: (Laa Ilaaha Illallaah. Wahdahuu Laa Shariika Lah. Lahulmulku walahulhamdu. Wahuwa Alaa Kulli Shai-in Qadiir).

Atafanya nini mtu ambaye hajahifadhi suratul faatiha na nyiradi za swala?

 • Ni wajibu wake kufanya juhudi ya kuhifadhi nyiradi za wajibu katika swala. Nyiradi hizo haziwi sahihi ispokuwa tu kwa lugha ya Kiarabu, nazo ni hizi:
  Suratul faatiha, Takbira, Sub-haana Rabbiyal-adhiim, Samiallahu Liman-hamidah, Rabbanaa Lakalhamdu, Sub-haana Rabbiyal-aalaa, Rabbighfir-lii, Tashahudi, Kumswalia Mtume, Assalaamu Alaykum Warahmatullaah.
  Ni wajibu kwa Muislamu katika swala zake kabla ya kukamilisha kuhifadhi akariri nyiradi anazozijua ikiwa ni pamoja na Tasbihi, Tahmidi na Takbira wakati wa kuswali, au kurudia kusoma aya anayo ihifadhi wakati wa kusimama. Amesema Allah kuwa: “Mcheni Allah kadiri muwezavyo”. (Sura Attaghaabun, aya 16)
 • Katika kipindi hiki anatakiwa kufanya bidii kubwa ya kuswali swala ya Jamaa ili aweze kuidhibiti swala yake, na ni kwa sababu imamu anabeba kiasi fulani cha mapungufu ya maamuma.
 • Katika Adhana ya Alfajiri ataongeza “Asswalaatu Khairun Minan-naum, Asswalaatu Khairun Minan-naum” baada ya “Hayya Alalfalaah”.

Mwongozo Mwepesi wa Muislam

Mtandao wa Mwongozo Mwepesi wa Muislam ni kitabu cha Mtandaoni cha kitabu asili ‘Mwongozo Mwepesi wa Muislam’ ambacho ni moja ya mradi wa Kampuni ya Mwongozo wa Kisasa na kimetolewa katika Lugha Zaidi ya 15 na maudhui yake yameambatana na ujuzi mkubwa wa kimtandao katika kufikisha.

Modern Guide