You are here

Vigawanyo

×

Error message

Deprecated function: Function create_function() is deprecated in views_php_handler_field->pre_render() (line 202 of /var/www/drupal7-websites/sites/all/modules/contrib/views_php/plugins/views/views_php_handler_field.inc).

Ujumbe wa Mitume wote kwa watu wao umeafikiana juu ya kumuabudu Allah pekee asiyekuwa na mshirika, na kuwakataa wale wanaobudiwa badala ya Allah. Hii ndio hakika ya maana ya Laa ilaaha Ilallah (hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allah tu), Muhammad Rasuulullah (Muhammad ni Mjumbe wa Allah). Na...

Allah amemuamrisha Muislamu kuusafisha moyo wake uondokane na maradhi ya nyoyo, kama: husda, kiburi na mfundo. Pia kuusafisha mwili wake uondokane na najisi na uchafu. Muislamu akifanya hayo, atastahiki kupata mapenzi ya Allah, kama Allah alivyosema kwamba: «Kwa yakini, Allah anawapenda wenye...

Swala ndio nguzo kubwa ya dini na ni mafungamano ya mja na Mola wake. Kwa sababu hiyo, swala imekuwa ibada kubwa sana na yenye hadhi tukufu mno. Allah amemuamrisha Muislamu kudumu kuswali katika mazingira yake yote; awapo mjini mwake, safarini, wakati wa afya njema na wakati wa ugonjwa. Maana ya...

Allah amefaradhisha kwa Waislamu kufunga mwezi mmoja katika mwaka. Ni mwezi wa Ramadhan uliobarikiwa. Ameufanya kuwa ni nguzo ya nne katika nguzo za Uislamu na ni katika majengo yake makubwa. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Enyi ambao mmeamini, imefaradhishwa kwenu funga kama ilivyo faradhishwa kwa...

Allah amefaradhisha Zaka na kuifanya nguzo ya tatu katika nguzo za Uislamu, amemuahidi adhabu kali mwenye kuacha kutoa Zaka, ameufungamanisha udugu wa Kiislamu kwa kutubu, kuswali na kutoa zaka, kama Allah alivyosema kuwa: «Ikiwa watatubu na wakasimamisha swala na wakatoa zaka, basi hao ni ndugu...

Kuhiji Makka ni nguzo ya tano katika nguzo za Uislamu, na ni ibada inayo kusanya aina kadhaa za ibada za kimwili, kiroho na mali. Ni wajibu kutekeleza kwa mwenye uwezo wa mali na afya mara moja tu katika umri.Allah amesema kuwa: «Na ni wajibu kwa watu kwa ajili ya Allah kuhiji Nyumba (Tukufu ya...

Kifo sio mwisho wa mambo, lakini ni hatua mpya kwa mwanadamu na ni mwanzo wa maisha kamili ya Akhera. Uislamu kama ulivyo fanya hima kubwa ya kuzilinda haki tangu wakati wa binadamu kuzaliwa ndivyo pia ulivyo weka mkazo wa sheria ambazo zinalinda haki za maiti na kuangalia hali za familia yake na...

Tabia njema katika Uislamu sio jambo la anasa wala la ziada. Tabia njema ni sehemu muhimu inayofungamana na dini katika pande zake zote. Tabia na maadili mema katika Uislamu yana nafasi na daraja la juu sana. Linadhihirika wazi hilo katika hukumu na sheria zote za Kiislamu. Mtume, swallalahu...

Uislamu umeweka kanuni na sheria zote ambazo zinamlida mwanadamu na pia kulinda haki zake za mali na kazi; sawa mwanadamu awe tajiri au masikini. Pia kanuni na sheria hizi zina mchango katika kuifanya jamii iwe na mashikamano na na maendeleo katika nyanja zote za maisha. Asili ya miamala ni...

Chakula halali kina nafasi kubwa katika Uislamu. Chakula halali ni sababu ya kukubaliwa kwa dua na baraka katika mali na familia. Makusudio ya chakula halali ni kile kitu ambacho ni chakula, halali, kilichopatikana kwa njia halali na kwa mali halali, bila ya kudhulumu au kupora haki za wengine....

Mavazi ni neema miongoni mwa neema za Allah kwa watu. Allah Mtukufu amesema kuwa: ‘‘Enyi wanadamu, kwa yakini kabisa tumekuteremshieni nguo zinazositiri tupu zenu na nguo za urembo. Na vazi la uchamungu ndio bora zaidi. Hizo ni miongoni mwa neema za Allah ili (wanadamu) wapate kukumbuka’’.(Al-...

Uislamu umetilia mkazo sana kuiimarisha familia na kuilinda dhidi ya mambo yanayoweza kuidhuru na kuhatarisha uwepo wake, kwa sababu kuimarika kwa familia ndio kuimarika kwa mtu mmoja mmoja na jamii kwa jumla. Ndoa katika Uislamu Hakiza mume na mke Ndoa ya matala (mke zaidi ya mmoja) Talaka...

Kumtaja Allah ni mojawapo ya ibada zenye malipo makubwa sana na zenye manufaa kwa mja duniani na akhera na, kwa sababu yake, mja anazidi kupata hadhi na kuwa karibu na Muumba wake Mtukufu. Nafasi ya uradi Nyiradi bora zaidi Hakika ya dua Taratibu za dua

Mwongozo Mwepesi wa Muislam

Mtandao wa Mwongozo Mwepesi wa Muislam ni kitabu cha Mtandaoni cha kitabu asili ‘Mwongozo Mwepesi wa Muislam’ ambacho ni moja ya mradi wa Kampuni ya Mwongozo wa Kisasa na kimetolewa katika Lugha Zaidi ya 15 na maudhui yake yameambatana na ujuzi mkubwa wa kimtandao katika kufikisha.

Modern Guide