You are here

Nyiradi katika mazingira tafauti

×

Error message

Deprecated function: Function create_function() is deprecated in views_php_handler_field->pre_render() (line 202 of /var/www/drupal7-websites/sites/all/modules/contrib/views_php/plugins/views/views_php_handler_field.inc).

Nyiradi za asubuhi na jioni

Aya Kursiy. Tazama uk.271

Sura za kinga. Tazama ukurasa 273

Kwa jina la Allah ambaye pamoja na jina lake hakiwezi kuleta madhara kitu chochote ardhini wala mbinguni na yeye ndiye tu Msikivu, Mjuzi.

Mtume amefahamisha kwamba hakuna mja yeyote anaye isoma aya hii asubuhi na jioni ya kila siku mara tatu halafu akadhuriwa na kitu. (Tirmidhiy 3388)

Nimeridhia kwamba Allah ndiye Mola na Uislamu ndio dini na Muhammad, swallalahu alayhi wasalam, ndiye Nabii.

Mtume amesema kuwa: «Hakuna mja yeyote Muislamu anayesema wakati wa asubuhi na wakati wa jioni mara tatu kwamba: Nimeridhia kwamba Allah ndiye Mola na Uislamu ndio dini na Muhammad, swallalahu alayhi wasalam, ndiye Nabii isipokuwa kwamba ni haki kwa Allah kumridhisha mja huyo Siku ya Kiyama». (Ahmad 18967). 

Ewe Mola wangu, wewe ni Mlezi wangu. Hakuna anayestahiki kuabudiwa ila wewe tu. Umeniumba na mimi ni mja wako. Na mimi niko katika ahadi yako kadiri niwezavyo. Ninaomba hifadhi kwako unikinge na uovu wa niliyoyafanya. Ninakiri neema zako kwangu, na ninakiri dhambi zangu kwako. Kwa hiyo, nisamehe kwa sababu hakuna anayesamehe dhambi ila wewe tu. 

Mtume amesema kuwa: «Na mwenye kuisema dua hiyo mchana akiwa na imani nayo na akafa katika mchana wake huo kabla hajafika jioni, basi yeye ni miongoni mwa watu wa peponi. Na mwenye kuisema wakati wa usiku akiwa na imani nayo na akafa kabla ya kufika asubuhi, basi yeye ni miongoni mwa watu wa peponi». (Bukhariy 5947)

Tumefika asubuhi na ufalme ni wa Allah, na shukurani anazistahiki Allah. Hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allah tu peke yake, akiwa hana mshirika. Ni wake yeye tu ufalme, na ni zake yeye tu shukurani, na yeye ni mwenye uwezo wa kila kitu. Ewe Mola wangu, ninakuomba kheri za yaliyomo katika mchana huu na kheri za yaliyomo baada yake. Na ninakuomba hifadhi unikinge na uovu wa yaliyomo katika mchana huu na uovu wa yaliyomo baada yake. Ewe Mola wangu, ninaomba hifadhi kwako unikinge dhidi ya uvivu na uzee mbaya. Ewe Mola wangu, ninaomba hifadhi kwako unikinge dhidi ya adhabu ya moto na adhabu ya kaburini. (Muslim 2723)

Na akifika jioni atabadilisha maneno ya asubuhi kwa jioni.

Dua wakati wa kula

Kabla ya kula

«Anapokula chakula mmoja wenu aseme Bismillaah. Akisahau kusema hivyo mwanzo wa kula kwake aseme Bismillaahi Fii Awwalihii Wa-aakhirihii». (Tirmidhiy 1858, 3264)

 Wakati wa kumaliza kula

«Ambaye amekula chakula na akasema Shukrani anazistahiki Allah ambaye amenipa chakula hiki na kuniruzuku bila ya mbinu zangu wala nguvu (zangu) zitasamehewa dhambi zake za zamani». (Tirmidhiy 3458, Abudaudi 4023)

Dua za nyumbani

Wakati wa kuingia nyumbani

«Mmoja wenu anapoingia nyumbani kwake aseme: Ewe Mola wangu, kwa yakini mimi ninakuomba uingiaji wa kheri na utokaji wa kheri. Kwa jina la Allah tumeingia na kwa jina la Allah tumetoka na Allah mola wetu tunamtegemea. Halafu aisalimie familia yake». (Abudaudi 5096)

 Wakati wa kutoka nyumbani

«Kwa jina la Allah. Namtegemea Allah. Hakuna mbinu wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allah. Ewe Mola wangu,  ninaomba hifadhi kwako unikinge nisipotee au kupoteza, na nisipotoke au kupotosha, na nisidhulumu au kudhulumiwa, na nisiwe mjinga au kufanywa mjinga». (Abudaudi 5094, 5095)

Dua wakati wa kulala

Dua kabla ya kulala

“Bismikallaahumma amuutu wa ahyaah (Kwa jina lako ewe Mola wangu ninakufa na ninakuwa hai)”. (Bukhari, Hadithi Na. 5953 – Muslim, Hadithi Na. 2711)

Adhana na msikiti

Sheria inamtaka Muislamu kuiga anayoyasema Muadhini isipokuwa tu pale Muadhini anaposema «Hayya alasw-swalaah» au «Hayya Alalfalaah» yeye atasema: «Laa Hawla Walaa Quwwata Illaa Billaah»..

Halafu baada ya Adhana kumalizika atasema: «Ewe Mola wangu, Mlezi wa huu wito uliotmia na swala iliyo simama, mpe Muhammad Wasila na Fadhila na mfikishe kwenye hadhi ya kusifika ambayo umemuahidi». Mtume amempa habari njema mwenye kusema hayo kwamba: «utakuwa halali kwake uombezi wangu». (Bukhariy 589)    

Wakati wa kuingia msikitini

Kwa jina la Allah, na rehema na amani zimfikie Mtume wa Allah. Ewe Mola wangu, nisamehe dhambi zangu na nifungulie milango ya rehema zako. Na akitoka atasema: Kwa jina la Allah na rehema na amani zimfikie Mtume wa Allah. Ewe Mola wangu, nifungulie milango ya fadhila zako.

Baada ya swala ya faradhi

Astaghfirullaah Atayasema haya mara tatu

Ewe Mola wangu, wewe ni amani na amani inatoka kwako. Umetukuka ewe mwenye utukufu na ukarimu. (Muslim 591)

Halafu atamtakasa Allah mara 33 akisema «Subhaanallaah» na atamshukuru Allah mara 33 akisema «Alhamdu Lillaah» na atamtukuza Allah mara 33 akisema «Allaahu Akbar» na atahitimisha mara mia moja kwa kusema «Laa Ilaaha Illallaah. Wahdahuu Laa Shariika Lah. Lahulmulk Walahulhamd. Wahuwa Alaa Kulli Shay-in Qadiir». (Muslim 597) Mtume amempa habari njema mwenye kusoma uradi huu kwamba dhambi zake zitasamehewa hata kama zilikuwa (nyingi) kama povu la bahari. (Muslim 597)

Kusoma Aya Kursiy (Tazama Uk.271 )

Kusoma sura za kinga (Tazama Uk.273 )

Mwongozo Mwepesi wa Muislam

Mtandao wa Mwongozo Mwepesi wa Muislam ni kitabu cha Mtandaoni cha kitabu asili ‘Mwongozo Mwepesi wa Muislam’ ambacho ni moja ya mradi wa Kampuni ya Mwongozo wa Kisasa na kimetolewa katika Lugha Zaidi ya 15 na maudhui yake yameambatana na ujuzi mkubwa wa kimtandao katika kufikisha.

Modern Guide