You are here

Mgawanyo wa wanawake kwa mwanaume

×

Error message

Deprecated function: Function create_function() is deprecated in views_php_handler_field->pre_render() (line 202 of /var/www/drupal7-websites/sites/all/modules/contrib/views_php/plugins/views/views_php_handler_field.inc).

---------------------------------------------------------------------

Kwa mwanaume, mwanamke anagawanyika katika mafungu kadhaa:

  1. Mwanamke anakuwa mkewe:

Inafaa kwa mwanaume kumuangalia na kustarehe na mkewe wakati wowote atakao, na mwanamke naye pia ni hivyo hivyo kwa mumewe. Allah amemtaja mke kuwa ni vazi kwa mume, na mume naye ni vazi kwa mke, ikiwa ni kuonesha  picha nzuri ya mawasiliano ya kiroho, ya kihisia na kimwili kati yao. Amesema Allah Mutukufu kuwa: «Wao (wanawake) ni vazi kwenu na nyinyi ni vazi kwao…». (Albaqara, aya 187) (Tazama Uk.248)

  1. Mwanamke anakuwa mtukando kwa mwanaume:

Mwananke Mtukando ni kila mwanamke ambaye sio miongoni mwa maharimu zake, sawa awe ni miongoni mwa ndugu zake wa karibu, kama vile mtoto wa kike wa baba yake mdogo au mkubwa, na mtoto wa kike wa shangazi yake, au mtoto wa kike wa mama yake mdogo au mkubwa, au mtoto wa kike wa mjomba wake, au asiwe miongoni mwa ndugu zake wa karibu na akawa hana uhusiano naye wa ukoo au kuoleana.. 

Uislamu umeweka vidhibiti na kanuni ambazo zinadhibiti  uhusiano wa Muislamu na mwanamke Mtukando ili kulinda heshima na ili kuziba milango ya shetani kwa mwanadamu. Allah aliyemuumba mwanadamu anafahamu zaidi maslahi ya mwanadamu. Amesema Allah Mtukufu kuwa: «Hivi hajui yule aliye umba, na hali ya kuwa yeye ndiye tu Mjua siri, Mwenye khabari?» (Al-mulk, aya 14).

  1. Mwanamke awe miongoni wa maharimu wa mwanaume huyo:

Maana ya maharimu ni kila mwanamke ambaye ni haramu kwa mwanaume kumuoa, uharamu wa milele. Maharimu  ni hawa wafuatao:

Nasaba 1

Mama mzazi, au bibi mzaa baba au mzaa mama, kama mama wa mama au mama wa baba na kuendelea.

2 Binti wa kuzaa au Binti wa mtoto wa kiume au wa  kike na kuendelea. 
3 Ndugu wa kike wa baba mmoja mama mmoja, au ndugu wa kike wa baba mmoja au ndugu wa kike wa  mama mmoja.
4 Shangazi; ndugu wa kike wa baba, wa baba mmoja mama mmoja, au baba mmoja, au mama mmoja. Anaingia katika fungu hili pia shangazi wa baba na shangazi wa mama.
5 Ndugu wa kike wa mama; wa baba mmoja mama mmoja, au ndugu yake wa baba mmoja, au wa mama mmoja. Anaingia katika kundi hili mama mdogo au mkubwa wa baba na mama mdogo au mkubwa wa mama.
6 Binti wa ndugu wa kiume, wa baba mmoja mama mmoja, au wa baba mmoja, au wa mama mmoja, na kuendelea kama vile binti wa mtoto wa kiume wa ndugu wa kiume.
7 Binti wa ndugu wa kike, wa baba mmoja mama mmoja, au wa baba mmoja, au wa mama mmoja, na kuendelea, kama vile binti wa mtoto wa kike wa ndugu wa kike.
Ukwe 8 Mama wa mke, sawa mke yuko naye au ametalikiana naye. Mama wa mke ni miongoni mwa wanawake ambao ni haramu uharamu wa milele kumuoa. Kadhalika ni haramu kumuoa mama wa mama mkwe (bibi).
9 Binti wa kufikia.
10 Mke wa mtoto wa kiume na kuendelea, kama vile mke wa mjukuu.
11 Mke wa baba na kuendelea kama vile mke wa baba wa baba (babu wa upande wa baba) au mke wa baba wa mama (babu wa upande wa mama).
Kunyonyesha 12

Mama wa kunyonya. Huyu ni mwanamke ambaye aliwahi kumnyonyesha wakati wa utotoni katika miaka miwili tangu kuzaliwa kwake. Awe alimnyonyesha mara tano zilizo shibisha. Uislamu umelifanya suala hilo ni haki kwa mwanamke huyo  kwa sababu ya kumnyonyesha.  

13

Ndugu wa kike wa kunyonya. Huyu ni binti wa mwanamke ambaye amemnyonyeshe mwanaume wakati wa utoto wake kama ilivyotangulia kuelezwa. Pia ndugu wote wa kunyonya wanakuwa haramu kama wanavyokuwa haramu ndugu wa nasaba, kama vile shangazi, mama mdogo au mkubwa, binti wa ndugu wa kiume na binti wa ndugu wa kike wa kunyonya. 

Mwongozo Mwepesi wa Muislam

Mtandao wa Mwongozo Mwepesi wa Muislam ni kitabu cha Mtandaoni cha kitabu asili ‘Mwongozo Mwepesi wa Muislam’ ambacho ni moja ya mradi wa Kampuni ya Mwongozo wa Kisasa na kimetolewa katika Lugha Zaidi ya 15 na maudhui yake yameambatana na ujuzi mkubwa wa kimtandao katika kufikisha.

Modern Guide