You are here

Lengo la kuwepo kwetu

×

Error message

Deprecated function: Function create_function() is deprecated in views_php_handler_field->pre_render() (line 202 of /var/www/drupal7-websites/sites/all/modules/contrib/views_php/plugins/views/views_php_handler_field.inc).
man pray in the mosque

Watu wengi mabingwa wa kufikiri na watu wa kawaida kwa pamoja wanakanganyika katika kujibu swali muhimu katika maisha yetu:

Kwa nini sisi tupo ulimwenguni?

Ni lipi lengo la maisha yetu?

Kwa yakini na kwa uwazi kabisa Qur’an imeliainisha lengo la kuwepo kwa mwanadamu katika haya maisha, katika kauli ya Allah isemayo kuwa: «Na sikuumba majini na watu isipokuwa tu waniabudu» (Sura Adh-dhaariyaat, aya 56). Hivyo, kuabudu ndio lengo la kuwepo kwetu katika hii dunia. Yasiyokuwa hayo ni nyenzo tu na vifuatishi.

Lakini ibada katika Uislamu sio utawa na kuyakimbia maisha na mambo yake matamu .Pia ibada, pamoja na swala, swaumu na zaka inajumuisha pia vitendo vyote vya mwanadamu na kauli zake, uvumbuzi wake, mahusiano yake; bali hata kucheza kwake na starehe zake, madamu yote hayo yataambatana na nia njema na makusudio mazuri. Na kwa sababu hii ndio Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Na katika utupu wa mmoja wenu kuna sadaka». Kwa maneno hayo, Mtume  swallalahu alayhi wasalam alikuwa na maana kwamba Muislamu anapata malipo na thawabu hata kwa kustarehe na mke wake.

Kwa sababu hiyo, ibada pamoja na kuwa lengo la maisha, inakuwa ndio maisha yenyewe. Kwa hiyo, Muislamu anaishi kati ya aina mbali mbali za ibada, kama Allah  alivyosema kuwa: «Sema: kuswali kwangu na kuchinja kwangu na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allah Mola wa walimwengu» (Sura Al-an’aam, aya 162).

Mwongozo Mwepesi wa Muislam

Mtandao wa Mwongozo Mwepesi wa Muislam ni kitabu cha Mtandaoni cha kitabu asili ‘Mwongozo Mwepesi wa Muislam’ ambacho ni moja ya mradi wa Kampuni ya Mwongozo wa Kisasa na kimetolewa katika Lugha Zaidi ya 15 na maudhui yake yameambatana na ujuzi mkubwa wa kimtandao katika kufikisha.

Modern Guide