You are here

Katika Uislamu hakuna aliye/kilicho kati baina ya mja na mola wake

×

Error message

Deprecated function: Function create_function() is deprecated in views_php_handler_field->pre_render() (line 202 of /var/www/drupal7-websites/sites/all/modules/contrib/views_php/plugins/views/views_php_handler_field.inc).

Dini nyingi zimewapa baadhi ya watu fulani hadhi ya kidini kuliko wengine na kufungamanisha ibada na imani zao na ridhaa za hao wachache na kukubali kwao. Wao, kwa mujibu wa dini hizo, ni wakaakati baina yao na baina ya Allah, nao ni miongoni mwa wanaotoa msamaha na wakati mwingine wanajua Ghaibu  (mambo yasiyoonekana kwa macho) – kama yalivyo madai yao batili – na wanaona kwamba kuwapinga ni sababu ya kupata hasara ya wazi. 

Uislamu umekuja na kumpa heshima mwanadamu na kuiweka juu hadhi yake, na kubatilisha kwamba wema wa mwanadamu au kutubu kwake au ibada zake zinafungamanishwa na watu maalumu, hata kama wamefikia kiwango gani cha ubora na wema.

Ibada za Muislamu ni kati yake yeye na Allah. Hakuna mtu yeyote mwenye fadhila katika ibada hizo au uingiliaji kati. Allah yuko karibu na waja wake; anasikia maombi ya mja na anamjibu. Anaona ibada zake na swala zake na anampa thawabu zake juu ya ibada hizo. Hakuna mtu yeyote anayemiliki haki ya kutoa msamaha na toba. Wakati wowote mja anapotubu na kumsafishia nia Allah Allah humkubalia toba yake na humsamehe. Hakuna yeyote mwenye nguvu zisizokuwa za kawaida wala uwezo wa kuwa na athari katika ulimwengu. Mambo yote yapo mkononi mwa Allah.

Uislamu umeikomboa akili ya mwanadamu na kumtaka afikiri, atumie akili na kutumia sheria za Qur’ani na kauli sahihi za Mtume swallalahu alayhi wassalam na matendo yake wakati wa kutofautiana. Hakuna mtu yeyote anayemiliki haki ya moja kwa moja na kuwajibika kufuata amri zake katika yote anayoyasema isipokuwa tu Mtume wa Allah, kwa kuwa yeye hatamki kutokana na mapenzi ya nafsi yake. Hakuna vingine isipokuwa kwamba anatamka kwa Wahyi na maelekezo ya Allah, kama Allah alivyosema kuwa: «Na hatamki kutokana na matamanio ya nafsi. Hayakuwa hayo (ayatamkayo) isipokuwa tu ni Wahyi unaotumwa» (Sura Annajmi, aya 3-4). 

Ni neema kubwa ilioje kwetu kwa kuwa na dini hii inayowiana na maumbile katika nafsi, inayomheshimu mwanadamu, inayomfanya ajiheshimu na inayomkomboa asiabudu na asinyenyekee vitu vingine badala ya Allah alietukuka na alie juu.

Mwongozo Mwepesi wa Muislam

Mtandao wa Mwongozo Mwepesi wa Muislam ni kitabu cha Mtandaoni cha kitabu asili ‘Mwongozo Mwepesi wa Muislam’ ambacho ni moja ya mradi wa Kampuni ya Mwongozo wa Kisasa na kimetolewa katika Lugha Zaidi ya 15 na maudhui yake yameambatana na ujuzi mkubwa wa kimtandao katika kufikisha.

Modern Guide