You are here

Mazingatio ni hakika ya Uislamu na sio hali za baadhi ya waislamu

×

Error message

Deprecated function: Function create_function() is deprecated in views_php_handler_field->pre_render() (line 202 of /var/www/drupal7-websites/sites/all/modules/contrib/views_php/plugins/views/views_php_handler_field.inc).

Ukimuona daktari anafanya jambo linalodhuru afya au mwalimu mwenye tabia mbaya, basi wewe pamoja na kushangaa kwako na kuchukizwa kwako na vitendo vyake vinavyopingana na elimu yake, taaluma yake na hadhi yake hutabadilisha msimamo wako kwamba elimu ya tiba ni muhimu kwa binadamu au kwamba elimu ni muhimu kwa jamii na kwa maendeleo.

Na utaona kwamba daktari huyo au mwalimu huyo si vingine isipokuwa kwamba ni mfano usipoendeza kwa taaluma na kazi anayohusika nayo.

Tukiona vitendo vibaya kwa baadhi ya Waislamu, hilo haliwakilishi hakika ya Uislamu ulio safi, lakini hicho ni kielelezo cha udhaifu wa kibinadamu na utamaduni na tabia mbaya ambazo hazina uhusiano wowote na Uislamu, kama ambavyo tabia za daktari huyo na mwalimu vitendo vyao havihusishwi na udaktari na ualimu.

Mwongozo Mwepesi wa Muislam

Mtandao wa Mwongozo Mwepesi wa Muislam ni kitabu cha Mtandaoni cha kitabu asili ‘Mwongozo Mwepesi wa Muislam’ ambacho ni moja ya mradi wa Kampuni ya Mwongozo wa Kisasa na kimetolewa katika Lugha Zaidi ya 15 na maudhui yake yameambatana na ujuzi mkubwa wa kimtandao katika kufikisha.

Modern Guide