You are here

Dini inagusa nyanja zote za maisha

×

Error message

Deprecated function: Function create_function() is deprecated in views_php_handler_field->pre_render() (line 202 of /var/www/drupal7-websites/sites/all/modules/contrib/views_php/plugins/views/views_php_handler_field.inc).

Uislamu sio hitajio la kiroho wanalolifanya Waislamu misikitini kwa kuomba dua na kusali tu.

Na pia sio maoni na itikadi pekee ambazo wafuasi wake wanaziamini.

Kama ambavyo pia sio tu mfumo kamili wa kiuchumi.

Na sio kanuni na nadharia tu za kujenga mfumo na jamii.

Vilevile sio maadili na tabia pekee katika mashirikiano na watu wengine

Lakini Uislamu ni mfumo kamili wa nyanja zote za maisha kwa upana wake na upeo wake wote. Unayajumuisha hayo na mengineyo.

Allah ameitimiza kwa Waislamu neema hii na kuiridhia kwetu dini hii iliyo kamilifu, kama alivyosema kuwa: «…leo nimekukamilishieni dini yenu na nimetimiza kwenu neema yangu na nimeridhia kwenu Uislamu kuwa ndio dini». (Sura Almaida, aya 3)

Na wakati kafiri mmoja alipomwambia Swahaba Salman Alfarsiy kwa kumkejeli kwamba: «Mwenzenu (akimkusudia Mtume wa Allah) anakufundisheni kila kitu hata taratibu za kwenda haja kubwa na haja ndogo? Swahaba alimjibu kuwa: «Ndio, ametufundisha». Halafu akamtajia sheria za Uislamu na taratibu zake katika suala hili. (Muslim, Hadithi Na. 262)

Mwongozo Mwepesi wa Muislam

Mtandao wa Mwongozo Mwepesi wa Muislam ni kitabu cha Mtandaoni cha kitabu asili ‘Mwongozo Mwepesi wa Muislam’ ambacho ni moja ya mradi wa Kampuni ya Mwongozo wa Kisasa na kimetolewa katika Lugha Zaidi ya 15 na maudhui yake yameambatana na ujuzi mkubwa wa kimtandao katika kufikisha.

Modern Guide