You are here

Uislamu ndio dini ya wastani

×

Error message

Deprecated function: Function create_function() is deprecated in views_php_handler_field->pre_render() (line 202 of /var/www/drupal7-websites/sites/all/modules/contrib/views_php/plugins/views/views_php_handler_field.inc).

Uislamu ni dini ya wastani, isiyokuwa na udekezaji na uzembe au ugumu na uchupaji wa mipaka. Haya yapo wazi katika masuala yote ya dini na ibada zake.

Na ni kwa sababu hii umekuja msisitizo wa  Allah kwa Mtume, swallalahu alayhi wasalam, kwa maswahaba wake na kwa Waumini kwa kuwataka wawe na msimamo wa wastani. Hilo lipatikane kwa kuzingatia mambo mawili:

Allah  amesema kuwa: «Kuwa imara kama ulivyoamrishwa; (wewe) na yule aliyetubu pamoja nawe, na msichupe mipaka. Kwa yakini, yeye anayaona mnayoyafanya». (Sura Huud, aya 112).

Maana ni kwamba: Jilazimishe kuwa imara katika haki na fanya juhudi katika hilo bila ya kuchupa mipaka na kupitiliza kwa kuongeza au kujifanya.

Mtume wa Allah, swallalahu alayhi wasalam, alipokuwa akiwafundisha masawahaba wake mojawapo ya matukio ya ibada ya Hija, aliwatahadharisha wasiwe na uchupaji wa mipaka na kuwazindua kwamba hiyo ni sababu ya kuangamia kwa mataifa yaliyopita. Amesema: «Jihadharini na kuchupa mipaka katika dini, kwani kumewaangamiza wale waliokuwepo kabla yenu kuchupa mipaka katika dini». (Ibnimaaja, Hadithi Na. 3029).

Na ni kwa sababu hii, ndio Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «jilazimisheni katika amali (kufanya) yale mnayoyaweza». (Bukhariy, Hadithi Na. 1100).

Mtume wa Allah, swallalahu alayhi wasalam,, ameweka wazi hakika ya ujumbe uliotumwa kwamba haukuja ili kuwakalifisha watu kufanya yaliyo nje ya uwezo wao. Si vingine isipokuwa kwamba ujumbe huo umekuja kufundisha, kutumia busara na kuwepesisha. Amesema: «Kwa yakini, Allah hakunituma niwe mwenye kuweka ugumu au niwe mgumu, na lakini amenituma niwe mfundishaji, muwepesishaji». (Muslim, Hadithi Na. 1478).

Mwongozo Mwepesi wa Muislam

Mtandao wa Mwongozo Mwepesi wa Muislam ni kitabu cha Mtandaoni cha kitabu asili ‘Mwongozo Mwepesi wa Muislam’ ambacho ni moja ya mradi wa Kampuni ya Mwongozo wa Kisasa na kimetolewa katika Lugha Zaidi ya 15 na maudhui yake yameambatana na ujuzi mkubwa wa kimtandao katika kufikisha.

Modern Guide