You are here

Nitazijua vipi Sheria za dini?

×

Error message

Deprecated function: Function create_function() is deprecated in views_php_handler_field->pre_render() (line 202 of /var/www/drupal7-websites/sites/all/modules/contrib/views_php/plugins/views/views_php_handler_field.inc).

Mtu aliyepata maradhi na akataka kuyatibu maradhi hayo, atamtafuta daktari bingwa sana na mjuzi sana ili achukue kwake tiba muafaka, na hatafanya uzembe wa kuchukua cheti chochote kwa daktari yeyote, kwa sababu maisha yake ni kitu ghali na cha thamani kwake.

Dini ya Muislamu ni kitu ghali sana katika vitu  anavyomiliki. Kwa hiyo, ni wajibu wake kuijua dini yake na kuuliza asichokijua kwa wanachuoni wenye ujuzi na uaminifu.

Kusoma kwako kitabu hiki ni hatua ya kukuweka katika njia sahihi, kama Allah aliye juu alivyosema kuwa: «…basi waulizeni wenye kujua ikiwa nyinyi hamjui». Suratu Annahli, aya 43. Ni wajibu wako kuendelea kufuata hatua nyingine likikutatiza jambo katika mambo ya dini kupitia vituo vya Kiislamu na Misikiti  iliyosimimishwa kwa misingi ya Qur’an na Sunna kwa ufahama wa wema waliopita iliopo karibu nawe. Unaweza kujua tovuti zake na anuani zao za mawasiliano kwa kutembelea kwako tovuti hii

Kama ambavyo pia unatakiwa kutembelea tovuti za mitandao zinazoaminika na ambazo zinafundisha masuala sahihi ya dini, mfano:

www.imuslimguide.com
www.newmuslimguide.com
www.al-islam.com
www.islamweb.net

Mwongozo Mwepesi wa Muislam

Mtandao wa Mwongozo Mwepesi wa Muislam ni kitabu cha Mtandaoni cha kitabu asili ‘Mwongozo Mwepesi wa Muislam’ ambacho ni moja ya mradi wa Kampuni ya Mwongozo wa Kisasa na kimetolewa katika Lugha Zaidi ya 15 na maudhui yake yameambatana na ujuzi mkubwa wa kimtandao katika kufikisha.

الدليل المعاصر