You are here

×

Error message

Deprecated function: Function create_function() is deprecated in views_php_handler_field->pre_render() (line 202 of /var/www/drupal7-websites/sites/all/modules/contrib/views_php/plugins/views/views_php_handler_field.inc).

Jambo kubwa kabisa kwa mwanadamu katika maisha yake ni kumuabudu Allah na kumtii
katika maamrisho yake na makatazo yake,katika hilo kuna mafanikio ya duniani na akhera, na
fahamu ya kuwa dini yote ni nyepesi, dini yote ndio kheri na dini yote ndio mafanikio.

Kumuabudu Allah kunajumuisha nyanja zote za maisha na inatakiwa ibada hizo ziwe kwa
elimu na ufahamu ili mwanadamu apate malipo kamili na aepukane na upotevu na kukosea.
Allah amesema kuwa: “Yeyote anayetaraji kukutana na Mola wake atende matendo mema na
asimshirikishe yeyote katika kumuabudu (kumtumikia) Mola wake”. Matendo mema ni yale
ambayo yamo katika njia sahihi kama Allah alivyoamrisha katika kitabu chake na kama Mtume
swallalahu alayhi wasalam alivyotufundisha. Kheri yote ipo katika kumfuata Mtume na kutenda
kwa mujibu wa mafundisho yake na mwongozo wake.

Muislamu kujifunza sheria za dini yake ni katika neema na tunu kubwa sana toka kwa Allah.
Mtume swallalahu alayhi wasalam amesema kuwa: “Yeyote ambaye Allah anamtakia kheri
humpa ufahamu katika dini”.

Katika kitabu hiki tumejitahidi kugusa mambo yote muhimu ya Uislamu ikiwa ni pamoja na
fikra, itikadi, sheria na maadili kwa kutumia njia nyepesi, yenye maana ya wazi na iliyopangwa
hatua kwa hatua pamoja na picha zinazo ongezea ufahamu na uzingatiaji katika maana ili kitabu
hiki kiwe rejea na hoja ya kitaaluma na chenye mvuto kwa Waislamu kwa taaluma zao tofauti.

Kwa msaada wa Allah utakuta kwamba kitabu ulicho nacho kinaiga mfumo wa Qur’ani katika
kutaja sheria za dini. Hakikujikita tu katika kutaja mambo yanayopasa kutendwa au kuachwa
lakini zaidi ya hapo kimekwenda mbali zaidi kwa kutaja roho ya ibada hizo, madhumuni yake
na athari yake. Pia kinajibu maswali muhimu sana katika kujifunza dini, hasa katika wakati huu
wenye mabadiliko ya haraka. Mfano: Kwa nini? Vipi? Inakuwaje, hali ikibadilika?

Tunamuomba Allah azifanye safi nia zetu, ayafanye mema matendo yetu na kutuongoza tuwe
na tabia nzuri, kauli nzuri na vitendo vizuri. Hakuna awezae kuongoza kwenye mazuri hayo
isipokuwa yeye tu. Pia tunamuomba atuepushe tusiwe na tabia mbaya, kauli mbaya na vitendo
vibaya. Hakuna awezaye kutuepusha na maovu hayo isipokuwa yeye tu. Na Tunamuomba Allah
kama alivomuamrisha Mtume wake swallalahu alayhi wasalam amuombe kwa kusema: “Ewe
Mola wangu, nizidishie elimu”. (Sura Twaha, aya 114)

Mwongozo Mwepesi wa Muislam

Mtandao wa Mwongozo Mwepesi wa Muislam ni kitabu cha Mtandaoni cha kitabu asili ‘Mwongozo Mwepesi wa Muislam’ ambacho ni moja ya mradi wa Kampuni ya Mwongozo wa Kisasa na kimetolewa katika Lugha Zaidi ya 15 na maudhui yake yameambatana na ujuzi mkubwa wa kimtandao katika kufikisha.

Modern Guide