You are here

Adhana

×

Error message

Deprecated function: Function create_function() is deprecated in views_php_handler_field->pre_render() (line 202 of /var/www/drupal7-websites/sites/all/modules/contrib/views_php/plugins/views/views_php_handler_field.inc).

Allah amewawekea Waislamu Adhana kwa ajili ya kuwaita watu katika swala, na kuwatangazia kuingia kwa wakati wake. Pia ameweka Iqama kwa ajili ya kuwatangazia juu ya kufika kwa wakati wa kuanza kwa swala. Waislamu  walikuwa wanakusanyika na kuswali katika nyakati zake bila ya kuwepo yeyote aliyekuwa akiitolea taarifa swala. Siku moja walilijadili jambo hilo. Baadhi yao walisema kuwa: «Wekeni kengele kama kengele za Wakristo». Wengine wakasema kuwa: «Hapana! Wekeni tarumbeta kama matarumbeta ya Wayahudi». Omar akasema kuwa: «Hivi mnaonaje mkimtuma mtu akawa anawatangazia watu swala?». Mtume ,swallalahu alayhi wasalam, akasema kuwa: «Ewe Bilali, simama na ita (watu) kwenye swala». (Bukhari, Hadithi Na. 579.   Muslim, Hadithi Na. 377)

Namna ya Adhana na Iqama

  • Adhana na Iqama ni lazima katika swala za Jamaa, si kwa mtu anayesali peke yake. Kama watu wata acha kuadhini na kuqimu kwa makusudio swala yao ni sahihi lakini watapata dhambi.
  • Sheria inataka Adhana itolewe kwa sauti nzuri na kubwa ili watu wasikie na waje kuswali.
  • Zimethibiti kunukuliwa namna  mbalimbali za Adhana na Iqama kutoka kwa Mtume,swallalahu alayhi wasalam. Maarufu zaidi ya namna hizo ni hizi zifuatayo:

Adhana:

«Laa Hawla Walaa Quwwata Illaa Billaah». Maana yake ni kwamba: Hatuna nguvu na uwezo wa kufanya ibada isipokuwa tu kwa kuwezeshwa na Allah.    

1 Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar.  (Allah ni mkubwa sana, Allah ni mkubwa sana, Allah ni mkubwa sana, Allah ni mkubwa sana). 
2 Ash-Hadu Al-Laa-Ilaaha Illallah, Ash-Hadu An-Laa-Ilaaha Illallah (Ninakiri kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah tu, Ninakiri kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah tu).
3 Ash-Hadu Anna Muhammadan Rasuulullah, Ash-Hadu Anna Muhammadan Rasuulullah, (Ninakiri kuwa Muhammad ni Mtume wa Allah, Ninakiri kuwa Muhammad ni Mtume wa Allah).
4 Haiyya Ala-Sswalaa, Haiyya Alaa-Sswalaa (Njooni kuswali, njooni kuswali).
5 Haiyya Alal-Falaah, Haiyya AlalFalaah. (Njooni kwenye mafanikio, njooni kwenye mafanikio).
6 Allahu Akbar, Allahu Akbar.(Allah ni mkubwa sana, Allah ni mkubwa sana).
7 Laa-Ilaaha Illallah.(Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah tu).
  • Katika Adhana ya Alfajiri ataongeza “Asswalaatu Khairun Minan-naum, Asswalaatu Khairun Minan-naum” baada ya “Hayya Alalfalaah”.

Iqama: 

1 Allahu Akbar, Allahu Akbar.(Allah ni mkubwa sana, Allah ni mkubwa sana).
2 Ash-Hadu Al-Laa-Ilaaha Illallah, (Ninakiri kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah tu).
3 Ash-Hadu Anna Muhammadan Rasuulullah, (Ninakiri kuwa Muhammad ni Mtume wa Allah).
4 Haiyya Ala-Sswalaa, (Njooni kuswali, njooni kuswali).
5 Haiyya Alal-Falaah. (Njooni kwenye mafanikio).
6 Qad Qaamatis-swalaa, qad qaamatis-swalaa. (Hakika, swala imesimama, hakika swala imesimama).
7 Allahu Akbar, Allahu Akbar.( Allah ni mkubwa sana, Allah ni mkubwa sana).
8 Laa ilaaha illa-llaah.( Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah tu).

Kusema kama anavyosema Muadhini

Inapendekezwa kwa anayesikia Adhana aseme kama Muadhini anavyosema, isipokuwa Muadhini atakapo sema: (Haiyya Alaas-swalaa, (Njooni kuswali,) au (Haiyya Alal-Falaah. (Njooni kwenye mafanikio) yeye atasema: (Laa haula walaa quwwata illaa billaah) (Hakuna ujanja (wa kufanya mema) wala nguvu (ya kuepuka maovu) isipokuwa kwa uwezo wa Allah tu).

Halafu aliyeisikia Adhana na baada ya kuikariri atasema: «Allahumma Rabba hadhihid-dawati-ttaamma waswalaatil-qaaimma aati Muhamadan alwasiilata walfadhiila wab-ath-hu maqaaman mahamuudan alladhii wa-attahu) (Ewe Mola wangu, Bwana wa wito huu uliotimia, na swala yenye kusimama, mpe Muhammad wasila na fadhila na mfikishe katika sehemu yenye kusifika ambayo umemuahidi.)

Mwongozo Mwepesi wa Muislam

Mtandao wa Mwongozo Mwepesi wa Muislam ni kitabu cha Mtandaoni cha kitabu asili ‘Mwongozo Mwepesi wa Muislam’ ambacho ni moja ya mradi wa Kampuni ya Mwongozo wa Kisasa na kimetolewa katika Lugha Zaidi ya 15 na maudhui yake yameambatana na ujuzi mkubwa wa kimtandao katika kufikisha.

الدليل المعاصر