You are here

Mambo matano ya msingi

×

Error message

Deprecated function: Function create_function() is deprecated in views_php_handler_field->pre_render() (line 202 of /var/www/drupal7-websites/sites/all/modules/contrib/views_php/plugins/views/views_php_handler_field.inc).

Hayo ni mambo makubwa ambayo mwanadamu hana budi kuyapata ili aishi maisha ya heshima, na sheria zote zimekuja ili kuamrisha mambo hayo yalindwe na kukataza yasivunjwe.

Umekuja Uislamu kuyalinda ili Muislamu aishi akiwa na amani na utulivu, akifanya mambo  kwa ajili ya dunia yake na akhera yake.

Na ili jamii ya Kiislamu iishi ikiwa taifa moja lenye mshikamano kama jengo, baadhi yake likiishikilia baadhi nyingine, na kama mwili; kiungo kimoja kikiugua mwili mzima unataabika kwa homa na kukesha. Kuyalinda mambo hayo kunapatikana kwa kufanya mambo mawili:

Kuyatekeleza na kuyalea.

Kuyalinda yasichezewe na yasiharibiwe.

Mambo hayo matano ya msingi ni kama ifuatavyo:

Dini:

Hili ni suala kubwa ambalo Allah  amewaumba binadamu kwa ajili yake na kuwatuma Mitume ili waifikishe na kuilinda, kama Allah alivyosema kuwa: «Na, kwa yakini kabisa, tumepeleka katika kila taifa Mtume akiwa na ujumbe kwamba: Muabuduni Allah na muepukeni twaghut». (Sura Annahli, aya ya 36)

Uislamu umechunga sana kuilinda dini na kuikinga dhidi ya kila jambo linaloichafua na kuuathiri usafi wake, ikiwemo shirki, mambo ya kubuni na uzushi au maasi na mambo ya haramu..

Mwili:

Allah ameamrisha kuilinda nafsi ya mwanadamu hata kama hilo litasababisha kufanya jambo la haramu, kwa sababu jambo hilo wakati wa dharura linasameheka, kama Allah alivyosema kuwa: «…basi aliyeshikika akiwa hajachupa mipaka, hakuna dhambi kwake. Kwa yakini, Allah ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa rehema». (Sura Albaqara, aya 173).

Pia Allah amekataza kuua mtu na kumdhuru. Amesema: «Na msiitupe mikono yenu kwenu mangamivu». (Sura Albaqara, aya 195).

Na ameweka adhabu ambazo zinazuia kuwadhuru watu bila ya haki, vyovyote dini yao iwavyo. Amesema: «Enyi ambao mmeamini, kimefaradhishwa kwenu kisasi katika waliouawa». (Sura Albaqara, aya 178). 

Akili:

Allah amekataza kila kitu kinachodhuru akili na utambuzi, kwakuwa akili ni mojawapo ya neema kubwa sana za Allah kwetu. Akili ndio muhimili wa heshima ya mwanadamu na ndio hadhi yake, na akili ndio wigo wa uwajibikaji na kuhesabiwa duniani na akhera.

Na kwasababu hii, Allah ameharamisha pombe na dawa za kulevya za aina zake zote, na kufanya kuwa ni uchafu mambo hayo katika vitendo vya shetani, na kusema kuwa: «Enyi ambao mmeamini, hakuna vingine isipokuwa kwamba pombe na kamari na masanamu na ramli ni uchafu katika vitendo vya shetani. Basi viepukeni ili mfaulu». (Sura Almaaida, aya 90).

Uzazi: 

Msisitizo wa Uislamu katika kulinda uzazi na kujenga familia ambayo mtoto katika familia hiyo analeleka katika maadili mema unaonekana dhahiri katika sheria nyingi. Miongoni mwa sheria hizo ni hizi:

•    Uislamu umehimiza kuoa, umefanya kuoa  jambo jepesi na kutofanya gharama zake kuwa kubwa. Allah amesema kuwa: «Na waozesheni wasio oa au kuolewa miongoni mwenu». (Sura Annuur, aya 32).

•    Uislamu umeharamisha mahusiano yote  ya haramu na kuziziba njia zote zinazoelekea kwenye mahusiano hayo.Allah amesema kuwa: «Na msiikaribie Zinaa, kwani ni jambo chafu na ni njia mbaya». (Sura Al-israi, aya  32).

•    Uislamu umekataza kuwatuhumu watu katika nasaba zao na heshima zao. Umelifanya jambo hilo kuwa miongoni mwa madhambi makubwa, na kumuwekea anayetenda hilo adhabu maalum duniani, achilia mbali adhabu itakayomkuta akhera.

•    Uislamu umeamrisha kuichunga heshima ya mwanaume na mwanamke, na kumhesabu mtu aliyeuawa akiitetea heshima yake na heshima ya familia yake ni Shahidi katika njia ya Allah. (Angalia uk 242).

Mali:

Uislamu umefanya ni wajibu kuhangaika katika kutafuta riziki ili kupata mali na umehalalisha miamala, kubadilishana vitu na pia biashara.

Na ili kuilinda mali, Uislamu umeharamisha riba, wizi, kughushi, kuvunja uaminifu na kula mali za watu kwa dhulma. Allah kamuahidi katika Qur’an anayefanya hayo atapata adhabu kali sana. (Angali uk. 206).

Mwongozo Mwepesi wa Muislam

Mtandao wa Mwongozo Mwepesi wa Muislam ni kitabu cha Mtandaoni cha kitabu asili ‘Mwongozo Mwepesi wa Muislam’ ambacho ni moja ya mradi wa Kampuni ya Mwongozo wa Kisasa na kimetolewa katika Lugha Zaidi ya 15 na maudhui yake yameambatana na ujuzi mkubwa wa kimtandao katika kufikisha.

الدليل المعاصر