You are here

Kujifundisha Sheria za Uislamu

×

Error message

Deprecated function: Function create_function() is deprecated in views_php_handler_field->pre_render() (line 202 of /var/www/drupal7-websites/sites/all/modules/contrib/views_php/plugins/views/views_php_handler_field.inc).

Inatakikana kwa Muislamu kuwa na bidii ya kujifundisha hukumu za sheria katika nyanja zote za maisha yake; katika ibada zake, miamala na mahusiano yake, ili atekeleze ibada kwa kujua na ufahamu, kama Mtume, swallalahu alayhi wasalam, alivyosema kuwa: «Mtu ambaye Allah anamtakia kheri humpa ufahamu katika dini». (Bukhari, Hadithi Na. 71 na Muslim, Hadithi Na. 1037).

Kwa hiyo, ni wajibu kwake kujifunza sheria zilizo wajibu kwake, kama: namna ya kusali, kujitoharisha, vyakula na vinywaji vya halali na vya haramu n.k. Pia inapendekezwa kwake kujifunza hukumu zinazohimizwa katika sheria lakini sio za wajibu kwake.

Hukumu za Sheria

Kauli zote za mwanadamu, vitendo vyake na harakati zake katika sheria hazitakuwa nje ya hali tano zifuatazo:

Wajibu

Hili ni jambo ambalo Allah ameamrisha lifanywe, kwa msingi kwamba anayelifanya anapewa thawabu na anayeacha kulifanya anastahiki adhabu. Mfano: kuswali Swala tano na kufunga Ramadhani.

Haramu

Ni jambo ambalo Allah amelikataza, kwa msingi kwamba anayeacha kulifanya anapewa thawabu na anayelifanya anastahiki adhabu, kama kuzini na kunywa pombe.

Sunna na Mustahabu

Hili ni jambo ambalo Uislamu unapendekeza lifanywe, kwa msingi kwamba anayelifanya anapewa thawabu na anayeacha kulifanya haadhibiwi. Mfano: kutabasamu mbele ya watu, kuanza kuwasalimia, kuondoa uchafu barabarani.

Makuruhu

Hili ni jambo ambalo Uislamu unahimiza liachwe, kwa msingi kwamba anapewa thawabu anayeacha kulifanya na haadhibiwi anayelifanya. Mfano: kuchezea vidole wakati wa kusali.

Mubaha

Hili ni jambo ambalo kulifanya na kuacha kulifanya hakufungamani na maamrisho au makatazo. Mfano: Kula, kunywa na kuzungumza.

Nguzo tano za Uislamu

Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Umejengwa Uislamu juu mambo matano: Kukiri kuwa hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah pekee na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allah , na kusimamisha Swala na kutoa zaka na kuhiji Nyumba Tukufu ya Allah(iliyopo Makka) na kufunga (mwezi wa) Ramadhani». (Bukhariy, Hadithi Na. 8,  na Muslim, Hadithi Na. 16) 

Nguzo hizi tano ndio misingi ya dini na nguzo zake kubwa. Tutazifafanua na kufasiri sheria zake katika sura zijazo.

Ya mwanzo ni kuamini na kupwekesha, na hii ndio sura inayokuja kwa anuani ya «Imani yako».

Inakuja baada yake swala ambayo ni ibada kubwa zaidi na ya kipekee sana. Mtume,swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «…na nguzo yake ni swala». (Tirmidhiy, Hadithi Na. 2749), kwa maana kwamba nguzo ya Uislamu ambayo unajengeka juu yake, na kwamba hakuna Uislamu bila ya kuwepo kwake ni Swala.

Lakini Swala, ili iwe sahihi, inashartiwa Muislamu aitekeleze akiwa katika Twahara. Kwa sababu hii, itaifuatia sura ya «Imani yako» sura ya «Twahara yako» halafu «Swala yako».

Nguzo za Uislamu

  1. Kukiri kuwa hakuna anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah pekee na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allah
  2. Kusimamisha swala
  3. Kutoa zaka
  4. Kufunga (mwezi wa) ramadhani
  5. Kuhiji Nyumba Tukufu ya Allah (iliyopo Makka

Mwongozo Mwepesi wa Muislam

Mtandao wa Mwongozo Mwepesi wa Muislam ni kitabu cha Mtandaoni cha kitabu asili ‘Mwongozo Mwepesi wa Muislam’ ambacho ni moja ya mradi wa Kampuni ya Mwongozo wa Kisasa na kimetolewa katika Lugha Zaidi ya 15 na maudhui yake yameambatana na ujuzi mkubwa wa kimtandao katika kufikisha.

الدليل المعاصر