You are here

Uislamu ni dini ya maisha

×

Error message

Deprecated function: Function create_function() is deprecated in views_php_handler_field->pre_render() (line 202 of /var/www/drupal7-websites/sites/all/modules/contrib/views_php/plugins/views/views_php_handler_field.inc).

Uislamu ni dini inayoweka uwiano baina ya maisha ya duniani na maisha ya akhera. Dunia ni shamba ambalo Muislamu anapanda mimea ya kheri katika nyanja zote za maisha, ili avune malipo  duniani na Akhera. Upandaji huu wa mimea unahitaji kuyakabili maisha kwa moyo wa matumaini uliojaa bidii na ari.Na hayo yanadhihirika katika mambo yafuatayo:

Kuistawisha dunia

Allah amesema kuwa: «Yeye amekuumbeni mwanzo kutokana na ardhi na kukutakeni mustawishe (maisha) humo» (Sura Huud, aya 61). Allah ametuumba katika hii ardhi na ametuamrisha tuistawishe na kuiendeleza kwa mambo ambayo yanawahudumia wanadamu, na yasiyopingana na sheria nzuri za Uislamu. Bali umefanya kuistawisha dunia na kuiendeleza ni miongoni mwa malengo na ni miongoni mwa ibada, hata katika mazingira magumu sana. Kwa sababu hii, Mtume, swallalahu alayhi wasalam, anamtanabahisha Muislamu kwamba anapokuwa katika hatua ya kupanda mche wa mmea na Kiama kikatokea, ni wajibu wake kufanya haraka kupanda mche huo, ikiwa ataweza, ili kwake iwe sadaka. (Almusnad, Hadithi Na. 2712).  

Kuchanganyika na watu

Uislamu unatoa wito kwa watu kushirikiana katika kujenga jamii, maendeleo, kufanya mema na kuchanganyika pia kuwasiliana kwa viwango vya juu sana vya tabia na maadili mazuri, pamoja na kutofautiana kwa dini zao na tamaduni zao. Pia Uislamu unatoa angalizo kwamba kukaa kando na kujitenga na watu sio njia ya walinganiaji (wahubiri) na watengenezaji mambo. Kwa sababu hii, Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amemfanya mtu ambaye anachanganyika na watu na kuvumilia maudhi yao na makosa yao ni bora zaidi kuliko yule mtu ambaye anajitenga na watu na kukaa mbali nao. (Ibnimaaja, Hadithi Na. 4032).

Dini ya elimu

Haikuwa bahati kwamba neno la kwanza katika Qur’an lililoteremka kwa Mtume, swallalahu alayhi wasalam, ni «Soma». Kwa hakika, umepatikana msisitizo katika  Uislamu kuzikubali aina zote za elimu yenye faida kwa mwanadamu, kiasi kwamba njia anayoifuata Muislamu katika kutafuta elimu na maarifa imekuwa ndio njia yake ya kumpeleka peponi, kama Mtume, swallalahu alayhi wasalam, alivyosema kuwa: «Yeyote anayefuata njia akitafuta elimu katika njia hiyo, Allah, kwa kufanya hivyo, humrahisishia njia katika njia za peponi». (Ibnihibban, Hadithi Na. 84)..

Uislamu haujawahi kutambua vita kati ya elimu na dini, kama ilivyo katika dini nyingine. Bali ni kinyume chake kabisa. Dini imekuwa ndio taa ya elimu na ndio nguzo yake na ndio inayotoa wito itafutwe kwa kujifunza na kufundisha, madamu katika elimu hiyo kuna kheri kwa wanadamu.

Kwa sababu hii, Allah ameitukuza hadhi ya mtu mwenye elimu anayewafundisha watu kheri, na amemvika taji la ngazi ya juu sana. Mtume, swallalahu alayhi wasalam, ameeleza kwamba viumbe vyote vinamuombea mema mtu anayewafundisha watu kheri. (Tirmidhiy, Hadithi Na. 2685).

Mwongozo Mwepesi wa Muislam

Mtandao wa Mwongozo Mwepesi wa Muislam ni kitabu cha Mtandaoni cha kitabu asili ‘Mwongozo Mwepesi wa Muislam’ ambacho ni moja ya mradi wa Kampuni ya Mwongozo wa Kisasa na kimetolewa katika Lugha Zaidi ya 15 na maudhui yake yameambatana na ujuzi mkubwa wa kimtandao katika kufikisha.

Modern Guide