You are here

Uislamu ni dini ya ulimwengu

×

Error message

Deprecated function: Function create_function() is deprecated in views_php_handler_field->pre_render() (line 202 of /var/www/drupal7-websites/sites/all/modules/contrib/views_php/plugins/views/views_php_handler_field.inc).

Dini ya Uislamu imekuja ikiwa rehema na muongozo kwa mataifa yote pamoja na tofauti za tamaduni,asili,desturi na nchi zao kama Allah alivyosema kuwa: «…na hatukukutuma wewe isipokuwa tu (ukawe) rehema kwa walimwengu» (Sura Al-anbiyaa, aya 107).

Na kwa sababu hii, Uislamu unaheshimu mila zote za watu na tamaduni zao, na hauwalazimishi Waislamu kuzibadilisha isipokuwa tu ikiwa zinapingana na jambo katika sheria za Uislamu. Mila inayopingana na Uislamu inapasa kuibadili kwa mila inayoafikiana nayo, kwa sababu Allah ambaye ameamrisha na kukataza ndiye mjuzi zaidi, na muktadha wa kumuamini kwetu Allah ni kufuata sheria zake.

Angalizo ni kufahamu kuwa mila za Waislamu ambazo hazina uhusiano na Uislamu na sheria zake Muislamu hatakiwi kisheria kuzifuata na kuzitekeleza. Hizo ni aina tu za mila za watu na maingiliano yao halali ya maisha.

Ardhi yote ni sehemu ya kumuabudu Allah 

Uislamu unaizingatia ardhi yote kuwa ni mahali panapofaa kuishi na kumuabudu Allah. Hakuna nchi au mahali maalumu ambapo ni wajibu kwa Waislamu kwenda na kuishi huko. Kinachozingatiwa ni uwezekano wa kumuabudu Allah.

Muislamu halazimiki kuhama kwenda sehemu nyingine ila tu kama amezuiwa kumuabudu Allah, likitokea jambo hilo atahama kwenda mahali atakapoweza kumuabudu Allah, kama Allah alivyosema kuwa: «Enyi waja wangu ambao mmeamini, kwa yakini, ardhi yangu ni pana, hivyo niabuduni mimi tu». (Sura Al-ankabuut, aya 56.)

Mwongozo Mwepesi wa Muislam

Mtandao wa Mwongozo Mwepesi wa Muislam ni kitabu cha Mtandaoni cha kitabu asili ‘Mwongozo Mwepesi wa Muislam’ ambacho ni moja ya mradi wa Kampuni ya Mwongozo wa Kisasa na kimetolewa katika Lugha Zaidi ya 15 na maudhui yake yameambatana na ujuzi mkubwa wa kimtandao katika kufikisha.

الدليل المعاصر