You are here

Namna ya kutoa zaka ya mifugo

×

Error message

Deprecated function: Function create_function() is deprecated in views_php_handler_field->pre_render() (line 202 of /var/www/drupal7-websites/sites/all/modules/contrib/views_php/plugins/views/views_php_handler_field.inc).

Kwanza: Ngamia

Zaka inakuwa wajibu katika aina zote za ngamia, ni sawa wawe na nundu moja au nundu mbili, endapo tu idadi yake itakuwa zaidi ya ngamia watano, kama jedwali ifuatayo inavyo onesha:

Idadi  Wajibu wa kutoa Idadi  Wajibu wa kutoa
Kuanzia Mpaka  Kuanzia Mpaka 
5 9 Mbuzi jike mmoja 36 45 Binti labuun
(Ngamia jike mwenye miaka miwili na akaingia wa tatu)
10 14 Mbuzi jike wawili 46 60 Hikka (Ngamia jike mwenye miaka miwili na akaingia wa nne)
15 19 Mbuzi jike watatu 61 75 Jidh’a(Ngamia  jike mwenye miaka minne na akaingia wa tano)
20 24 Mbuzi jike wanne 76 90 Binti labuun wawili (Ngamia jike mwenye miaka miwili na akaingia  wa tatu)
25 35 Binti Makhadh (Ngamia jike mwenye mwaka mmoja na akaingia  wa pili) 91 120 (Ngamia jike Mwenye miaka mitatu na akaingia wa nne)

Ngamia wakiwa zaidi ya mia na ishirini, wajibu kutoa zaka kwa kila ngamia arubaini ni ngamia jike mmoja ambaye ametimiza miaka miwili na kuingia mwaka wa tatu.  Na katika kila ngamia hamsini atatoa zaka ngamia jike mmoja ambaye ametimiza miaka mitatu na kuingia wa nne. Itafanyika hivyo kwa idadi yoyote itakayo ongezeka.

Pili: Ng`ombe

Zaka ni wajibu katika aina zote za jamii ya ng’ombe, kama vile nyati na wengine ikiwa idadi yake itazidi ng’ombe thalathini, kama ifuatavyo:

Idadi  Wajibu wa kutoa
Kuanzia Mpaka 
30 39 Ijili (Ng’ombe dume aliyetimiza mwaka mmoja kamili)
40 59 Musinna (Ng’ombe jike aliyetimiza miaka miwili kamili)
60 69 Ijili wawili (Kila mmoja awe ametimiza mwaka mmoja kamili)
70 79 Musinna (Aliyetimiza miaka miwili kamili) + Tabii (Aliyetimiza mwaka mmoja kamili)
80 ~ Ng’ombe wakifika thamanini na zaidi, katika kila ng’ombe 30 atatoa Tabii (aliyetimiza mwaka mmoja kamili), na katika kila ng’ombe arubaini, atatoa Musinna (aliyetimiza miaka miwili kamili).

Tatu: Mbuzi na kondoo

Zaka inakuwa wajibu katika jamii ya mbuzi na kondoo kwa aina zake zote, iwapo idadi yake itazidi arubaini, kama ifuatavyo:

Idadi  Wajibu wa kutoa
Kuanzia Mpaka 
40 120 Mbuzi jike mmoja
121 200 Mbuzi jike wawili
201 399 Mbuzi jike watatu
400 ~ Idadi ya mbuzi au kondoo ikifika 600, zaka yake ni kwamba katika kila mia moja ni mbuzi mmoja = Kwa maana hiyo, katika mbuzi 600 ni mbuzi 6, na katika mbuzi 700 ni mbuzi saba, n.k. 

Nani anapewa zaka?

Uislamu umeainisha maeneo ambayo zaka inatakiwa itumike. Inafaa kwa Muislamu kuiweka zaka katika eneo moja tu au zaidi miongoni mwa maeneo haya, au kuikabidhi kwa taasisi na jumuiya za Kiislamu ambazo itazigawa kwa Waislamu wanaostahiki kupewa. Jambo bora zaidi ni kuigawa zaka ndani ya mji (ambao mtoaji zaka anaishi). 

Makundi yanayostahiki kupewa zaka ni haya yafuatayo:

  1. Fukara na masikini: Hawa ni wale watu ambao hawana kipato kinacho watosheleza katika mahitaji yao ya lazima na ya msingi.
  2. Wanaofanya kazi ya kukusanya zaka na kuigawa. 
  3. Mtumwa ambaye anataka kujikomboa kutoka kwa mmiliki wake. Atasaidiwa na kupewa zaka ili ajikomboe na kuwa huru.
  4. Mtu ambaye ana mzigo wa deni na hawezi kulilipa. Ni sawa deni mtu alilichukua kwa manufaa ya jamii na kulenga kuwafanyia watu jambo jema au kwa manufaa yake binafsi.
  5. Wanaopigania dini ya Allah. Hawa ni wale watu wanaopigana kwa ajili ya kuilinda dini yao na nchi zao. Linaingia katika eneo hili kila jambo ambalo linalenga kuutangaza Uislamu na kulipa nguvu neno la Allah.
  6. Wanaolainishwa nyoyo zao. Hawa ni makafiri ambao wameingia katika Uislamu karibuni, au makafiri ambao kuna matarajio ya kuwa wanaweza kuingia katika Uislamu. Kundi hili halitakiwi kupewa zaka na mtu mmoja mmoja, bali kazi ya kuwapa zaka inatakiwa kufanywa na kiongozi wa Waislamu au taasisi za Kiislamu ambazo zitapima tija  katika kufanya hivyo.
  7. Msafiri mgeni ambaye amekwama na anahitaji fedha. Atapewa zaka hata kama yeye ni tajiri mjini kwake.

Allah akiainisha makundi yanayostahiki kupewa zaka amesema kuwa: «Hakuna vingine isipokuwa kwamba zaka ni ya fukara na masikini na wafanyakazi wa zaka na wanaolainishwa nyoyo zao na watumwa (wanaotaka kujikomboa) na wenye madeni na wanaopigania dini ya Allah na wasafiri». (Sura Attauba, aya 60).

Mwongozo Mwepesi wa Muislam

Mtandao wa Mwongozo Mwepesi wa Muislam ni kitabu cha Mtandaoni cha kitabu asili ‘Mwongozo Mwepesi wa Muislam’ ambacho ni moja ya mradi wa Kampuni ya Mwongozo wa Kisasa na kimetolewa katika Lugha Zaidi ya 15 na maudhui yake yameambatana na ujuzi mkubwa wa kimtandao katika kufikisha.

Modern Guide