You are here

Makusudio ya zaka

×

Error message

Deprecated function: Function create_function() is deprecated in views_php_handler_field->pre_render() (line 202 of /var/www/drupal7-websites/sites/all/modules/contrib/views_php/plugins/views/views_php_handler_field.inc).

Allah amefaradhisha zaka kwa Waislamu kwa malengo makubwa. Tunataja baadhi yake kama ifuatavyo:

  1. Kupenda mali ni jambo la kimaumbile kwa mwanadamu linalomfanya kuwa na ari kubwa ya kuihifadhi kuihangaikia. Sheria imelazimisha kutoa zaka ili kuisafisha nafsi iondokane na tabia chafu ya ubahili na tamaa, na ili kuondosha kuipenda  kuipapatikia dunia. Allah amesema kuwa: «Chukua kutoka katika mali zao zaka uwatakase na uwasafishe kwayo».  (Sura Attauba, aya 103)
  2. Kwa kutoa zaka unaimarika msingi wa kupendana na kushikamana, kwa sababu nafsi ya mwanadamu imeumbwa katika kumpenda anayeifanyia jambo zuri. Kwa kufanya hivyo, wanajamii ya Kiislamu wataishi kwa kupendana na kushikamana, kama jengo moja lililo imara ambalo lenyewe kwa lenyewe hujiimarisha. Pia vitendo vya wizi, uporaji na unyan’ganyi vitapungua. 
  3. Kupitia zaka, hupatikana maana halisi ya utumishi,  unyenyekevu na utiifu kamili kwa Allah Mola wa ulimwengu. Tajiri anapotoa zaka ya mali yake anatekeleza sheria na amri ya Mola wake. Katika kutoa zaka kuna kumshukuru Allah Mneemeshaji juu ya neema hiyo. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Kwa yakini kabisa, mkishukuru, nitakuongezeeni». (Sura Ibrahim, aya 7). 
  4. fulani baina ya makundi katika jamii. Kwa kutoa zaka na kuwapa wanaostahiki, rasilimali hazitarundikana katika mikono ya watu wachache na kujilimbikizia. Allah Mtukufu anasema kuwa: «…ili (mali hiyo) isije ikawa kinyan’ganyiro baina ya matajiri wenu tu». (Sura Al-hashri, aya7) 

Nafsi zimeumbwa na tabia ya kumpenda mwenye kuzifanyia mazuri.

Mwongozo Mwepesi wa Muislam

Mtandao wa Mwongozo Mwepesi wa Muislam ni kitabu cha Mtandaoni cha kitabu asili ‘Mwongozo Mwepesi wa Muislam’ ambacho ni moja ya mradi wa Kampuni ya Mwongozo wa Kisasa na kimetolewa katika Lugha Zaidi ya 15 na maudhui yake yameambatana na ujuzi mkubwa wa kimtandao katika kufikisha.

Modern Guide