You are here

Kuamini Mitume

×

Error message

Deprecated function: Function create_function() is deprecated in views_php_handler_field->pre_render() (line 202 of /var/www/drupal7-websites/sites/all/modules/contrib/views_php/plugins/views/views_php_handler_field.inc).

Watu kuhitaji Mtume na Mjumbe toka kwa Allah

Hakuna budi kwa watu kupata ujumbe wa Allah unaowabainishia sheria na kuwaongoza kwenye mambo ya sawa. Utume ni roho ya ulimwengu, ni nuru yake na ni uhai wake. Ulimwengu una wema gani iwapo utakosa roho, uhai na nuru?

Na ni kwa sababu ndio Allah ameuita ujumbe wake Roho. Roho ikikosekana uhai nao unakosekana. Allah amesema kuwa: «Na kama hivyo, tumeleta wahyi kwako; roho kutokana na amri yetu. Hukuwa ukijua ni nini kitabu wala imani. Na lakini tumeifanya iwe nuru tunamuongoza kwayo tumtakaye katika waja wetu». (Sura Ash-shuuraa, aya 52).

Hiyo ni kwa sababu akili, japokuwa inajua kutofautisha kati ya jema na baya kwa ujumla, isipokuwa kwamba haiwezi kujua uchambuzi wa hayo na vigawanyo vyake na namna kutekeleza ibada na namna zake isipokuwa tu kwa njia ya Wahyi na utume.

Hakuna njia ya kupata faraja na ufaulu wa duniani na Akhera isipokuwa tu kwa kupitia mikono ya Mitume, na hakuna njia ya kujua jema na baya kwa undani isipokuwa tu kwa kupitia njia yao. Yeyote anayepuuza ujumbe, itampata hali ya kutotulia,na pia watapata masikitiko kwa kiasi cha kuupinga kwake ujumbe na kuupuuza. 

Mojawapo ya nguzo za Imani:

Kuamini Mitume ni mojawapo ya nguzo sita za Imani. Allah amesema kuwa: «Mtume ameayaamini yale yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake, na waumini (pia wameyaamini). Wote wamemuamini Allah na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume wake. Hatubagui kati ya yeyote miongoni mwa Mitume wake». (Sura Albaqara, aya 285).

Aya imetoa ushahidi wa wajibu wa kuwaamini Mitume wote, Allah awafikishie amani, bila ya kubagua. Hatuamini baadhi ya Mitume na kuwakataa baadhi, kama ilivyo kwa Wayahudi na Wakristo.

Mtume, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuhusu Imani kwamba: «Ni wewe kumuamini Allah na Malaika wake na Vitabu vyake na Mitume wake na Siku ya Mwisho na (wewe) kuamini Qadari; kheri yake na shari yake». (Muslim, aya 8). 

Maana ya kuamini Mitume:

Ni Imani thabiti ya kuamini kwamba Allah katika kila uma amepeleka Mtume anayetokana na wao akiwalingania kumuabudu Allah pekee asiyekuwa na mshirika, na kwamba Mitume wote ni wakweli, wathibitishaji, wachamungu, waaminfu, viongozi, wenye kuongoka, na kwamba wao wameyafikisha yote ambayo Allah amewatuma. Hawakuficha, hawakubadilisha, hawakuongeza kutokana na matakwa yao na hawakupunguza, kama Allah alivyosema kuwa: «Hakuna la wajibu kwa Mitume isipokuwa tu kufikisha kuliko bayana». (Sura Annahli, aya 35).

Allah ametueleza kuwa hakuna umma wowote wa binadamu isipokuwa kwamba ameupelekea Mtume, na kwamba yeye Allah hamuadhibu yeyote madamu ujumbe haujamfikia.

Maana ya kuamini Mitume:

Ni Imani thabiti ya kuamini kwamba Allah katika kila uma amepeleka Mtume anayetokana na wao akiwalingania kumuabudu Allah pekee asiyekuwa na mshirika, na kwamba Mitume wote ni wakweli, wathibitishaji, wachamungu, waaminfu, viongozi, wenye kuongoka, na kwamba wao wameyafikisha yote ambayo Allah amewatuma. Hawakuficha, hawakubadilisha, hawakuongeza kutokana na matakwa yao na hawakupunguza, kama Allah alivyosema kuwa: «Hakuna la wajibu kwa Mitume isipokuwa tu kufikisha kuliko bayana». (Sura Annahli, aya 35).

Miujiza ya Mitume:

Allah amewatia nguvu Mitume wake kwa hoja na ushahidi mbali mbali unao onesha ukweli wao na kuwa wao ni Mitume. Miongoni mwa hayo ni kuwatia nguvu kwa miujiza ya wazi ambayo haiko katika uwezo wa binadamu, kwa minajli ya kuthibitisha ukweli wao na unabii wao.

Maana ya miujiza ni: Mambo yasiyokuwa ya kawaida anayo yaonesha Allah kupitia kwa Manabii  na Mitume wake, kwa namna ambayo wanadamu hawawezi kufanya kama hayo.

Miongoni mwa miujiza hiyo ni hii:

 • Kubadilishwa kwa fimbo ya Mtume Mussa, Allah amfikishie amani, kuwa nyoka.
 • Mtume Issa, Allah amfikishie amani, kuwapa taarifa watu sifa za chakula watakachokula na watachoweka akiba katika nyumba zao.
 • Kupasuka kwa mwezi, kwa Mtume wetu Muhammad, swallalahu alayhi wasalam.

Kuamini Mitume kunajumuisha nini?

 • Kuamini kwamba ujumbe wao ni wa kweli kutoka kwa Allah, na kwamba wito wa ujumbe wa Mitume wote umeafikiana katika kumuabudu Allah pekee asiyekuwa na mshirika, kama Allah alivyosema kuwa: «Na, kwa yakini kabisa, tumepeleka Mtume katika kila uma (akiwa na ujumbe) kwamba: Muabuduni Allah na muepukeni Twaqhuti». (Sura Annahli, aya 36). 

Na sheria zinaweza kutafautiana katika masuala tanzu yakiwemo halali na haramu kwa namna ambayo yanawiana na mataifa hayo, kama Allah alivyosema kuwa: «Kila (taifa) moja katika nyinyi tumeliwekea sheria na mfumo». (Sura Almaaida, aya 48).

 • Kuwaamini Mitume na Manabii wote. Tunawaamini Mitume ambao Allah amewataja kwa majina, mfano: Muhammad Ibrahimu, Mussa, Issa na Nuhu, Allah awafikishie amani. Ama wale Mitume ambao hatuyajui majina yao, tunawaamini kwa jumla. Yeyote anaye ukataa utume wa mmoja katika wao, basi anakuwa amewakataa wote.
 • Kuamini kuwa ni za kweli taarifa sahihi za Mitume na Miujiza yao katika Qur’ani na Suna, kama vile tukio la kupasuliwa kwa bahari kwa Mtume Mussa, Allah amfikishie amani.
 • Kuzitekeleza sheria za Mtume ambaye ametumwa kwetu, na ambaye ni Mtume bora zaidi miongoni mwa Mitume na ni wa mwisho wao. Huyo ni Muhammad, swallalahu alayhi wasalam.

Miongoni mwa sifa za Mitume:

 1. Wao ni binadamu. Tofauti kati yao na kati ya wanadamu wengine ni kwamba Allah amewapa jukumu maalumu la Wahyi na Utume. Allah amesema kuwa: «Na hatukuwatuma kabla yako isipokuwa tu wanaume tunaowapelekea Wahyi». (Sura Al-anbiyaa, aya 7).
  Hawana sifa yoyote ya Uungu na Umola. Wao ni binadamu ambao wamefikia kiwango cha juu cha ukamilifu katika umbo la nje, kama ambavyo pia wamefikia kiwango cha kabisa cha tabia kamilifu. Wao pia ni watu wenye nasaba bora sana. Wana akili kubwa na lugha fasaha kwa kiasi kinachowafanya wawe na sifa za kubeba majukumu ya Utume na kusimamia masuala mazito ya Unabii.
  Allah amewafanya Mitume kuwa wanatokana na wanadamu, ili kiigizo chao kiwe kinatokana na wao, na kwa sababu hiyo, kumtii Mtume na kumuiga linakuwa jambo ambalo limo ndani ya mipaka ya uwezo wao.
 2. Allah amewatua kwa kuwapa jukumu maalum la Utume. Allah amewateua wao tu kwa kuwapa wahyi, na kuwaacha watu wengine, kama Allah alivyosema kuwa: «Sema: Hakuna vingine isipokuwa kwamba sisi ni wanadamu tu kama nyinyi. Unaletwa Wahyi kwangu kwamba hakuna vingine isipokuwa kwamba Muabudiwa wenu wa haki ni mmoja tu». (Sura Alkahf, aya 110).
  Utume na Unabii haupatikani kwa usafi wa kiroho, werevu na akili za kimantiki. Ni uchaguzi na uteuzi wa Allah. Allah anawateua Mitume na kuwachagua na kuwaacha wanadamu wengine, kama alivyosema kuwa: «Allah anajua zaidi pale mahali anapoweka ujumbe wake». (Sura Al-an’aam, aya 124).
 3. Wamepewa kinga ya kutofanya makosa katika yale mambo wanayoyawasilisha kutoka kwa Allah. Hawakosei katika kuufikisha ujumbe utokao kwa Allah, na hawakosei katika kutekeleza yale ambayo Allah ameyafikisha kwao kwa njia ya Wahyi.
 4. Ukweli. Mitume, Allah awafikishie amani, ni wakweli katika kauli zao na vitendo vyao. Allah amesema kuwa: «Haya ndio yale ambayo (Allah) Mwingi wa rehema ameahidi, na Mitume wamesema kweli». (Sura Yasin, aya 52).
 5. Uvumilivu. Wamelingania kwenye dini ya Allah wakitoa habari njema na habari za maonyo, na huku wakikumbana na aina mbali mbali za maudhi na matatizo. Walivumilia na kuwa na subira katika kulifanya neno la Allah liwe juu. Allah Mtukufu amesema kuwa: «Kuwa mvumilivu kama walivyokuwa wavumilivu Mitume wenye msimamo». (Sura Al-ahqaaf, aya 35).

Matunda ya kuamini Mitume:

Kuamini Mitume kuna matunda adhimu, miongoni mwa matunda hayo ni haya:

 1. Kujua rehema ya Allah na kuwajali waja wake, kwa kule kuwapelekea Mitume ili wawaongoze kwenye njia sahihi, na kuwabainishia namna ya kumuabudu Allah. Hii ni kwa sababu, akili ya mwanadamu peke yake haiwezi kulijua hilo. Allah Mtukufu akimuelezea Mtume wetu Muhammad, swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Na hatukukupeleka wewe isipokuwa tu ukawe rehema kwa walimwengu». (Sura Al-anbiyaa, aya 107).
 2. Kumshukuru Allah kwa neema hii kubwa:
 3. Kuwapenda Mitume, Allah awafikishie rehema na amani, kuwaheshimu na kuwasifu kwa sifa zinazolingana na wao, kwa kuwa wao wamesimamia kuabudiwa kwa Allah, wamefikisha ujumbe wake na wamewanasihi waja wake.
 4. Kufuata ujumbe ambao Mitume wamekuja nao ukitoka kwa Allah, na ambao ni kumuabudu Allah pekee asiyekuwa na mshirika. Kwa kufanya hivyo, itapatikana kwa waumini kheri na uongofu katika maisha yao, na pia faraja duniani na akhera.

Allah Mtukufu amesema kuwa: «Basi yeyote aliyefuata muongozo wangu, hatapotea na hatataabika. Na yeyote aliyepuuza ukumbusho wangu, basi atapata maisha magumu». (Sura Twaha, aya 123 – 124). 

Mlima ambao unaitwa Mlima wa Mussa uliopo katika kisiwa cha Sinai na ambao baadhi ya watafiti wanasema kuwa ni mlima ambao Allah alizungumza na Mussa hapo.

Mwongozo Mwepesi wa Muislam

Mtandao wa Mwongozo Mwepesi wa Muislam ni kitabu cha Mtandaoni cha kitabu asili ‘Mwongozo Mwepesi wa Muislam’ ambacho ni moja ya mradi wa Kampuni ya Mwongozo wa Kisasa na kimetolewa katika Lugha Zaidi ya 15 na maudhui yake yameambatana na ujuzi mkubwa wa kimtandao katika kufikisha.

الدليل المعاصر