You are here

Swala ya jamaa

Allah amewaarimsha wanaume kuswali swala tano katika jamaa. Imethibiti kuwa malipo yake ni makubwa. Mtume,swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Swala ya jamaa ni bora zaidi kuliko swala ya mtu peke yake kwa daraja ishirini na saba». (Bukhari, Hadithi Na. 619- Muslim, Hadithi Na. 650).

Uchache wa idadi ya watu kuswali jamaa ni imamu na maamuma. Kila jamaa inapokuwa na watu  wengi sana basi inapendeza zaidi kwa Allah.

Maswahaba walikuwa na bidii ya kuswali swala ya Jamaa kiasi kwamba walikuwa wakizingatia kwamba kudumu kuacha swala ya Jamaa ni tabia miongoni mwa tabia za unafiki. 

Maana ya kumfuata imamu

Ni maamuma mwenye kuswali kuifungamanisha swala yake na imamu wake. Amfuate katika kurukuu kwake, kusujudu kwake na asikilize kisomo chake. Hatakiwi kumtangulia au kutofautiana naye katika jambo lolote katika hayo. Anatakiwa kufanya jambo mara tu  baada ya imamu wake kulifanya.

Mtume,swallalahu alayhi wasalam, amesema kuwa: «Hakuna vingine isipokuwa kwamba amewekwa imamu ili afuatwe. Akitoa Takbira basi nanyi toeni Takbira, na wala msitoe Takbira mpaka yeye atoe Takbira. Na atakapo rukuu nanyi rukuuni, na wala msirukuu mpaka yeye arukuu. Na akisema: Samia-llahu liman-hamidah, basi semeni Rabbanaa Walakal-hamdu. Na akisujudu basi sujuduni, na wala msisujudu mpaka yeye asujudu…».    (Bukhari, Hadithi Na. 701-  Muslim, Hadithi Na. 414-   Abuu daudi 603)

Nani anafaa kufanywa imamu?

Anatangulizwa kuwa imamu yule aliehifadhi zaidi Qur`ani, kisha anayefuatia, kisha anayefuatia, kama Mtume,swallalahu alayhi wasalam, alivyosema kuwa: «Awaongoze watu msomaji wao zaidi wa kitabu cha Allah. Ikiwa watakuwa sawa katika kusoma, aongoze mjuzi wao zaidi wa sunna..»  (Muslim, Hadithi Na. 673).

Imamu na maamuma wanasimamaje? 

Inatakiwa imamu awe mbele, na maamuma wajipange safu  nyuma yake, na wajaze safu moja baada ya nyingine.  Kama maamuma ni mmoja basi asimame upande wa kulia wa imamu.

Atakamilisha vipi kilicho mpita kwa imamu?

Yeyote atakaye unga swala kwa imamu huku akiwa amepitwa na kitu katika swala, basi atamfuata imamu mpaka atoe salamu, kisha akamilishe kilicho mpita katika swala yake.

Pale alipomkuta imamu huhesabiwa kuwa ndio mwanzo wa swala yake, na atakayo yafanya baada ya hapo huhesabiwa kuwa ndio mwisho wa swala yake.

Vipi rakaa huwahiwa?

Swala huhesabiwa kwa idadi ya rakaa, na mwenye kuwahi rukuu pamoja na imamu hakika ameiwahi rakaa ikiwa kamili. Mwenye kupitwa na rukuu basi ataungana na imamu, lakini yale matendo na maneno yaliyo baki ya rakaa hiyo  hayatahesabiwa katika rakaa zake (ameikosa rakaa).

Mifano ya maamuma ambaye amepitwa na kitu mwanzo wa Swala pamoja na imamu.

  • Mwenye kuwahi rakaa ya pili pamoja na imamu katika swala ya Alfajiri basi itamlazimu, baada ya salamu ya imamu, asimame na akamilishe rakaa iliyompita. Hatakiwi kutoa salamu mpaka aimalize rakaa hiyo, kwa sababu swala ya Alfajiri ina rakaa mbili, na yeye hakuwahi isipokuwa rakaa moja tu.
  • Mwenye kumuwahi imamu akiwa katika Tashahudi ya Mwisho katika swala ya Magharibi basi itamlazimu, baada ya salamu ya imamu, asali rakaa tatu zote, kwa sababu amemkuta imamu akiwa katika Tashahudi, na rakaa inawahiwa kwa kuwahi kurukuu pamoja na imamu.
  • akimkuta imamu akiwa katika rukuu ya rakaa ya tatu katika swala ya adhuhuri  atakuwa amewahi rakaa mbili pamoja na imamu ( hii ni Kutokana na maamuma kukosa rakaa mbili za mwanzo za swala ya adhuhuri) imamu atakapo toa salam itamlazimu(maamuma) kusimama na kukamilisha kilicho bakia, nazo ni rakaa mbili ya tatu na ya nne kwani adhuhuri ina rakaa nne.

Mwongozo Mwepesi wa Muislam

Mtandao wa Mwongozo Mwepesi wa Muislam ni kitabu cha Mtandaoni cha kitabu asili ‘Mwongozo Mwepesi wa Muislam’ ambacho ni moja ya mradi wa Kampuni ya Mwongozo wa Kisasa na kimetolewa katika Lugha Zaidi ya 15 na maudhui yake yameambatana na ujuzi mkubwa wa kimtandao katika kufikisha.

الدليل المعاصر